Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tisa wafariki kwa mkanyagano mkesha wa mwaka mpya

6DA8EDA1 A6B2 4701 9FC8 9CA7E7BE746C 1140x640.jpeg Tisa wafariki kwa mkanyagano mkesha wa mwaka mpya

Sun, 1 Jan 2023 Chanzo: dar24.comu

Takriban watu tisa wamefariki ,na wengine ambao idadi yao haikuweza kujulikana mara moja kujeruhiwa baada ya kutokea mkanyagano wakati wa shamrashamra za sherehe ya mwaka mpya jijini Kampala nchini Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi nchini Uganda, imesema baadhi ya waliofariki ni watoto waliokuwa wakihudhuria hafla hiyo ya burudani ndani ya jumba lenye maduka kando ya barabara kuu ya Kampala kuelekea Entebbe liitwalo Freedom City Mall.

Taarifa hiyo, imeeleza kuwa umati ulijitokeza kutazama onyesho la fataki majira ya usiku uliingia katika kadhia ya mkanyagano uliopelekea wengi wao kujeruhiwa na baadhi kufariki papo hapo na Hospitalini.

Aidha, Polisi inasema uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kilichotokea katika maonesho hayo ya fataki ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2023 yaliyoruhusiwa katika Taifa hilo.

Chanzo: dar24.comu