Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tisa wafariki kwa Kipindupindu Congo

Kipindu Pindu Congo Tisa wafariki kwa Kipindupindu Congo

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mara baada ya kutangaza kuitokomeza Ebola, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaripoti mlipuko mwingine wa Kipindupindu ambao hadi sasa umeua watu takribani tisa katika jimbo la Haut-Lomami.

Kundi la madaktari wasio na Mipaka (Médecins Sans Frontières) wametoa tahadhari ya kuongezeka kwa idadi ya vifo kufuatia ufinyu wa huduma muhimu za afya katika eneo hilo.

Hata hivyo mbinu za kupambana na kasi ya mlipuko huo zinaendelea kuchukuliwa na Wizara ya Afya ya nchini humio ili kuweza kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live