Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tisa wafariki, 80 walazwa kwa ugonjwa usiyojulikana Kenya

Tisa Wafariki, 80 Walazwa Kwa Ugonjwa Usiyojulikana Kenya Tisa wafariki, 80 walazwa kwa ugonjwa usiyojulikana Kenya

Thu, 11 May 2023 Chanzo: Bbc

Watu tisa wamefariki na wengine zaidi ya 80 kulazwa hospitalini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa usiojulikana katika kaunti ya Marsabit kaskazini mwa Kenya.

Msimamizi wa eneo hilo alisema kati ya watu tisa ambao wamekufa, sita walikuwa watu wazima na watoto watatu kati ya mwaka mmoja na mitatu.

Wengi wa watu walioathiriwa walionyesha dalili kama za mafua, macho ya manjano, wengu kuvimba na maumivu makali ya kichwa, vyombo vya habari vya nchini humo vinaripoti.

Baadhi ya wagonjwa wamepatikana na kuwa na malaria lakini madaktari wanasema huenda ni leishmaniasis ya visceral-pia inajulikana kama ugonjwa wa kala-azar .

Mlipuko huo unajiri miezi miwili baada ya Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu nchini Kenya kugundua mbu washambuliaji katika maeneo ya Laisamis na Saku kaunti ya Marsabit.

Chanzo: Bbc