Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tinubu kupiga marufuku safari za nje

Rais Tinubu Aachilia Huru Maelfu Ya Wafungwa Nigeria Tinubu kupiga marufuku safari za nje

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu ataweka marufuku ya miezi mitatu kwa mawaziri na maafisa wengine wa serikali kusafiri nje ya nchi kwa fedha za umma.

Mkuu wa Utawala, Ofisi ya Rais Tinubu amesema hatua hiyo imesbabishwa Rais kuwa na “wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa gharama za usafiri” kutokana na safari za maafisa wa serikali.

Marufuku hiyo itaanza Aprili 1. Rais Tinubu na utawala wake umeshutumiwa na baadhi ya watu kutokana na safari za mara kwa mara nje ya nchi.

Tangu alipoapishwa mwezi Mei 2023, Bwana Tinubu amefanya zaidi ya ziara 15 nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live