Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tinubu aongoza katika kinyang'anyiro cha urais wa Nigeria

Tinubu Aongoza Katika Kinyang'anyiro Cha Urais Wa Nigeria Tinubu aongoza katika kinyang'anyiro cha urais wa Nigeria

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Mgombea wa chama tawala Bola Ahmed Tinubu anaongoza uchaguzi mkuu wenye ushindani mkali zaidi nchini Nigeria tangu nchi hiyo irejee kwa demokrasia zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Majimbo 14 kati ya majimbo 36 hadi sasa yametangazwa rasmi na Tume Huru ya Uchaguzi. Bw Tinubu sasa amepata 47% ya kura zilizohesabiwa kufikia sasa.

Mgombea mkuu wa upinzani Atiku Abubakar anafuatia katika nafasi ya pili, akifuatiwa na Peter Obi wa Labour.

Ili kushinda urais, mgombea anahitaji kuwa na kura nyingi zaidi kwa jumla na kushinda 25% katika majimbo 25 kati ya 36 ya Nigeria.

Lakini mchakato wa uchaguzi umeingia katika utata.

Mapema Jumatatu, vyama vyote viwili vya upinzani vilitoka nje ya kituo cha kitaifa katika mji mkuu, Abuja, ambako matokeo yalikuwa yakitangazwa.

Walishutumu Tume Uchaguzi kwa ukosefu wa uwazi katika mfumo mpya wa kielektroniki wa wapiga kura, madai ambayo tume inakanusha.

Waangalizi wa Umoja wa Ulaya walisema mipango duni ya Tume Uchaguzi na mawasiliano yanadhoofisha imani katika mchakato huo.

Kura za maoni pia zimeshuhudia usumbufu mkubwa. Bw Tinubu alishindwa huko Lagos, ngome yake kwa zaidi ya miongo miwili, na mgombea wa chama cha tatu Peter Obi ambaye amepata uungwaji mkono miongoni mwa vijana wa Nigeria.

Bw Abubakar, mpinzani mkuu wa Bw Tinubu, alishinda Katsina, jimbo analotoka Rais anayeondoka Muhammadu Buhari ambaye anamuunga mkono Bw Tinubu.

Rais mpya wa Nigeria atakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kuzorota kwa usalama, ukosefu wa ajira na kudorora kwa uchumi.

Chanzo: Bbc