Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tinubu ameunda kikosi kazi cha kutafuta suluhu ya uchumi wa nchi

Tinubu Aanza Tinubu ameunda kikosi kazi cha kutafuta suluhu ya uchumi wa nchi

Thu, 28 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ametangaza kuundwa kwa kikosi kazi cha dharura chenye jukumu la kujaribu kutafuta suluhu ya uchumi wa nchi hiyo unaoendelea kushuka.

Bei za vyakula na bidhaa za mafuta zimeripotiwa kupanda, idadi kubwa ya raia wakionekana kukabiliwa na changamoto kutokana na mishahara yao midogo.

Matatizo makubwa ya kiuchumi yamechangia ugumu wa maisha hatua ambayo imeendelea kutoa shinikizo kubwa kwa utawala wa rais Tinubu kutafuta suluhu ya tatizo hilo.

Baadhi ya raia wa Nigeria wameituhumu serikali kwa kuondoa ruzuku ya mafuta , hatua ambayo imechangia kushuka kwa thamani ya sarafu ya nchi hiyo ,naira suala ambalo pia limetajwa kuchangia kupanda kwa gharama ya maisha.

Kikosi kazi hicho kinaundwa na maafisa wakuu wa serikali na viongozi wenye tajiriba katika nyanja tofauti.

Rais pia alianzisha baraza la rais la uratibu wa uchumi (PECC) ambalo atakuwa mwenyekiti na kusimamia mageuzi ya kiuchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live