Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tinubu aanza "mageuzi makubwa" ya sera ya ukusanyaji kodi

Tinubu Aanza Tinubu aanza "mageuzi makubwa" ya sera ya ukusanyaji kodi

Tue, 4 Jul 2023 Chanzo: Voa

Mamlaka ya mapato ya serikali ya Nigeria ilisema Jumatatu inashirikiana na chama cha wafanyabiashara kukusanya kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kutoka kwa mamilioni ya wafanyabiashara wasio rasmi, sehemu ya msukumo wa kupanua wigo wa kodi, wa serikali ya Rais Bola Tinubu.

Nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika imezanza kutekleza ajenda yake kubwa zaidi ya mageuzi katika miongo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa ruzuku ya petroli, iliyokuwa maarufu miiongoni mwa raia, na vikwazo vya biashara ya fedha za kigeni, katika juhudi za Tinubu za kujaribu kuimarisha uchumi uliodorora.

Nigeria ina mojawapo ya viwango vya chini zaidi vya ukusanyaji wa kodi duniani, ikikusanya takriban asili mia 10.8 ya Pato la Taifa, kulingana na Huduma ya serikali kuu ya Mapato ya Ndani ya Nchi (FIRS).

Ni asilimia 47 pekee ya ufadhili wa bajeti ya mwaka huu ambao utatokana na mapato. Asili mia 53 na itagharamiwa na mikopo.

FIRS ilisema katika taarifa yake kuwa inashirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Soko la Nigeria (MATAN) kukusanya na kutuma kodi ya VAT kutoka kwa wanachama wake, hasa wale walio katika sekta isiyo rasmi, kwa kutumia mfumo wa kidigitali.

Ilisema ushirikiano huo utasaidia "kuzuia shughuli za walaji rushwa, wabadhirifu na watoza kodi haramu ushuru katika masoko ya nchi hiyo.

Chanzo: Voa