Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi: Rais wa Burundi ataka kupinduliwa

Evariste Ndayishimiye Fg Evariste Ndayishimiye.

Thu, 8 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati hali ikionekana kuwa shwari, mvutano wa kisiasa umeongezeka tena, kufuatia tuhuma za baadhi ya viongozi wakuu kupanga njama ya kumng'oa madarakani Rais Evariste Ndayishimiye.

Mnamo Agosti 2, Rais Ndayishimiye, alipokuwa akiwahutubia maafisa wa Serikali alionya kuwa “baadhi ya watu” ambao hakuwataja wanatishia kupindua Serikali yake baada ya kuwa madarakani kwa miaka 2 tuu

Haya yanakuja ikiwa ni baada ya video kusambaa mtandaoni zikimuonesha Waziri Mkuu, Alain Guillaume Bunyoni akilalamika kuhusu viongozi wasengenyaji na kuibua hofu ya uwezekano wa mzozo wa madaraka kati ya viongozi hao

Ijumaa iliyopita, Rais Ndayishimiye, wakati akihutubia maofisa wa Serikali huko Gitega, aliwaonya baadhi ya watu wanaotaka kuiangusha Serikali yake ikiwa ni miaka miwili pekee akiwa ndani ya madaraka.

President Ndayishimiye, ambaye aliingia madarakani Juni, mwaka 2020, aliahidi kushughulika na mafisadi na watumishi wa umma wazembe aambapo mpaka sasa ameshawatimua watumishi wengi wa Serikali kwa kushindwa kuwa waadilifu.

Burundi wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali tangu kupata uhuru wao mwaka 1962, ambapo mwaka 2015 waandamanaji waliingia barabarani kupinga uongozi wa Rais aliyekuwepo madarakani, Pierre Nkurunziza yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000.

Kumekuwa na majaribio ya mara kwa mara ya kutaka kupindua Serikali ya Burundi ambapo mwaka….. waasi walitaka kumpindua Rais Nkurunziza akiwa nchini Tanzania, lakini jaribio hio lilizimwa na vyombo vya ulinzi na usalama na rais akarejea nchini mwake salama, ambapo watuhumiwa hao bado wanasota jela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live