Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetemeko Morocco: Nusu ya wakazi wa kijiji wamekufa au wamepotea

Tetemeko Morocco: Nusu Ya Wakazi Wa Kijiji Wamekufa Au Wamepotea Tetemeko Morocco: Nusu ya wakazi wa kijiji wamekufa au wamepotea

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Zaidi ya watu 2,000 wameuawa katika tetemeko kubwa la ardhi nchini Morocco siku ya Jumamosi.

Tulitembelea Tafeghaghte, kijiji kilichoharibiwa na tetemeko la ardhi la Morocco. “Watu wa kijiji hiki wapo hospitalini au wamekufa,” mkazi wa kwanza tuliyekutana naye kijijini hapo alisema kuhusu hali ilivyokuwa pale.

Tulipita juu ya kifusi na kugundua jinsi isingewezekana kwa mtu yeyote kutoka nje.

Matofali na mawe ya nyumba za kitamaduni katika kijiji hicho hayakuweza kustahimili ukubwa wa tetemeko hili mbaya la ardhi.

Watu 90 kati ya 200 wamekufa hapa. Huku wengine wengi wakiwa hawajulikani walipo.

"Hakuwa na wakati wa kutoka na kujiokoa," Hassan, ambaye aliweza kujiokoa kutoka kwenye vifusi vya majengo aliambia BBC.

Abdou Rahman anaonekana akiwa na mpwa wake. Mke wake na watoto watatu walikufa katika tetemeko la ardhi.Image caption: Abdou Rahman anaonekana akiwa na mpwa wake. Mke wake na watoto watatu walikufa katika tetemeko la ardhi.

Hassan alisema mjomba wake bado amezikwa chini ya vifusi. Sasa hakuna nafasi kwamba wanaweza kumtoka hai.

Hakuna aliye na vifaa vya uokoaji hapa.

"Mwenyezi Mungu ameleta haya na tunamshukuru kwa chochote tulichopata lakini sasa tunahitaji msaada wa serikali. Wamechelewa sana. Wamechelewa sana kuja kusaidia watu."

Chanzo: Bbc