Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tembo amkanyaga hadi kufa mwongozaji wa watalii Afrika Kusini

Tembo Amkanyaga Hadi Kufa Mwongozaji Wa Watalii Afrika Kusini Tembo amkanyaga hadi kufa mwongozaji wa watalii Afrika Kusini

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Wahifadhi wa mazingira wanaomboleza kifo cha mwongoza watalii wa Zimbabwe ambaye alikanyagwa hadi kufa na tembo aliyekuwa akimfukuza katika Hifadhi ya Kibinafsi ya Gondwana ya Afrika Kusini.

David Kandela, 36, alikuwa akiongoza kundi la watalii Jumapili jioni wakati mkasa huo ulipotokea, hifadhi hiyo ilisema katika taarifa iliyonukuliwa na vyombo vya habari vya ndani.

Iliongeza kuwa kisa hicho kilitokea wakati kundi moja la tembo wa Gondwana lilikuwa likipitia kambi ya Gondwana yenye mahema ya Eco Camp.

"Kundi hilo lilikuwa karibu kupita kambini wakati David alikutana na tembo wa mwisho aliyesalia kabla tu ya tukio hilo la kutisha," taarifa hiyo iliongeza.

Waelekezi na wasafirishaji wa watalii wamemtaja Bw Kandela kama kiongozi wa watalii mwenye taaluma ambaye aliipenda sana kazi yake.

Matukio kama haya ni nadra, lakini tembo wanadaiwa kusumbuliwa kwa urahisi na idadi kubwa ya watalii haswa katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa watalii wa safari.

Tembo ni kivutio kikubwa cha watalii kusini mwa Afrika.

Chanzo: Bbc