Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tatizo la kipindupindu Zimbabwe linachochewa na uhaba wa maji

Tatizo La Kipindupindu Zimbabwe Linachochewa Na Uhaba Wa Maji Tatizo la kipindupindu Zimbabwe linachochewa na uhaba wa maji

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Kwa miezi kadhaa sasa, Zimbabwe imekuwa ikipambana kukomesha kuenea kwa ugonjwa hatari wa kipindupindu katika miji na vijiji vyake kwa sababu nchi hiyo haina maji safi.

"Maji yakitoka kabisa mara nyingi huwa machafu," Regai Chibanda, baba wa watoto watano mwenye umri wa miaka 46 kutoka kitongoji cha Chitungwiza, aliniambia.

Kipindupindu, ni maambukizi makali ya kuhara yanayosababishwa na ulaji wa chakula au maji yaliyochafuliwa na bakteria Vibrio cholerae, unaweza kuenea haraka katika hali ya msongamano na chafu.

Imekuwa aina zimwi baya kwa taifa hili la kusini mwa Afrika - mwaka 2008-2009 zaidi ya 4,000 waliaga dunia wakati ugonjwa huo ulipotokea katika kipindi ambacho tayari kilikuwa na msukosuko .

Ilionyesha mzozo wa kisiasa na kiuchumi unaoendelea wakati mfumuko wa bei ulifikia asilimia 80 bilioni na kutangaza serikali ya kihistoria ya kugawana madaraka ambayo hatimaye ilikabiliana na hali hiyo.

Leo mfumuko wa bei unazidi kuibua tena makali yake na ugonjwa wa kipindupindu umeenea katika majimbo yote 10 ya nchi, ambayo yanaathiri zaidi watoto, mara nyingi huachwa bila uangalizi katika joto huku wazazi wao wanapojaribu kufanya kazi.

Mlipuko huu ulianza mnamo Februari na Oktoba ilipomalizika takwimu rasmi kutoka Idara ya Afya na Huduma ya Watoto zimeorodhesha karibu kesi 6,000 na vifo 123 vinavyoshukiwa.

Rais Emmerson Mnangagwa, ambaye alishinda uchaguzi wenye utata mwezi Agosti kwa muhula wa pili madarakani, ameahidi mpango wa nchi nzima wa kuchimba visima.

Hii itasaidiwa na vituo vya maji vinavyotumia nishati ya jua, hasa kuhudumia vijiji 35,000 ambavyo havina maji safi ya kunywa.

Katika mji mkuu, Harare, wakaazi wanaweza kukaa kwa wiki, au hata miezi, bila usambazaji wa maji wa kawaida kutoka kwa Halmashauri ya Jiji la Harare.Katika kitongoji cha Harare cha Chitungwiza, zaidi ya vifo 50 viliripotiwa mwishoni mwa mwezi Oktoba - wote kutokana na kipindupindu.

Chanzo: Bbc