Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tarehe ya kuzikwa kwa mwanahabari wa KBC Betty Barasa aliyeuawa yatangazwa

A4bafddbcb70dd0d Tarehe ya kuzikwa kwa mwanahabari wa KBC Betty Barasa aliyeuawa yatangaz

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Familia ya Betty Barasa imethibitisha kwamba atazikwa Jumatano, Aprili 14 nyumbani kwake mtaani Ngong' kaunti ya Kajiado

- Marehemu aliuawa kwa kupigwa risasi na genge la majambazi Jumatano, Aprili 7

- Makachero wa DCI hawajafanikiwa kukamata hata mshukiwa mmoja lakini uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo ya kinyama bado unaendelea

Aliyekuwa mhariri wa video katika Shirika la Utangazaji la KBC Betty Barasa anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake mtaani Ngong' Jumatano, Aprili 14 Kajiado.

Betty hadi kifo chake alikuwa na umri wa miaka 41.

Marehemu aliuawa kwa kupigwa risasi na majambazi Jumatano, Aprili 7 baada ya kurejea nyumbani kwake kutoka kazini.

Mwanahabari huyo alifika nyumbani mwendo wa saa mbili usiku ambapo genge la majambazi nilimvamia baada ya mjakazi kumfungulia lango kuu.

Genge hilo lilimfuata hadi eneo alokuwa ameegesha gari na kumlazimisha awapeleke ndani ya nyumba ambapo wanawe pamoja na mumewe walikuwa.

Kulingana na taarifa aliotoa kwa wanahabari, mjakazi wake alisema genge hilo lilitaka pesa na bidhaa zingine za thamani ikiwemo simu yake ya rununu.

Betty alipigwa risasi mara mbili kwenye kichwa kabla genge hilo kutoroka na simu yake pamoja na tarakilishi.

Hadi kufikia sasa, maafisa wa upelelezi hawajafanikiwa kumkamata mshukiwa hata mmoja lakini uchunguzi dhidi ya mauaji hayo ya kinyama unaendelea.

Aidha, wapelelezi wanaochunguza kifo cha mwanahabari huyo, wanaamini kwamba mauaji yake yalipangwa kwa sababu washambuliaji walionekana kumlenga yeye kati ya watu wengine sita ambao pia walikuwa ndani ya nyumba hiyo akiwemo rafiki yake.

Kulingana na uchunguzi wa upasuaji wa maiti yake, Betty alifariki dunia kutokana na risasi alilopigwa kichwani.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke