Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tarehe mpya ya uchaguzi yatangazwa Nigeria

Mtukura Februari 25 mwaka ujao uchaguzi utafanyika

Sun, 27 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya uchaguzi la Nigeria jana Jumamosi limetangaza kuahirisha uchaguzi wa Rais na wabunge wa 2023 kwa wiki moja, kutokana na kucheleshwa kupitishwa kwa sheria mpya ya uchaguzi.

Sheria hio mpya inaruhusu uhamishaji wa matokeo kielektroniki. Hatua ambayo inaweza kuboresha uwazi na kusaidia kuzuia udanganyifu katika nchi ambayo imekuwa ikikubwa na madai ya wizi wa kura mara nyingi.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Nigeria Mahmood Yakubu aliwaambia waandishi wa habari uchaguzi wa Rais na bunge la taifa sasa utafanyika Jumamosi tarehe 25 Februari 2023.

Rais Muhammadu Buhari, ambaye anatarajiwa kumaliza ngwe yake mwaka ujao baada ya kuhudumu kwa mihula miwili ya miaka minne, alitia saini muswada huo wa uchaguzi uliofanyiwa marekebisho siku ya Ijumaa, zaidi ya miezi saba baada ya kupitishwa na Baraza la Seneti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live