Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kuwa kitovu cha biashara maziwa makuu

76890d45f9cb4efbf7d41df1ab4b0093 Tanzania kuwa kitovu cha biashara maziwa makuu

Tue, 22 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TANZANIA inalenga kuwa kitovu cha biashara, usafi ri na usafi rishaji katika kanda nzima ya Maziwa Makuu na Afrika Mashariki.

Baadhi ya mikakati iliyowekwa serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ili kufikia azma hiyo ndani ya kipindi kifupi kijacho ni kununua meli mpya na kuzikarabati meli za zamani katika Ziwa Tanganyika kama Mv Liemba na Ziwa Victoria ili ziweze kufanya safari za ndani na katika ukanda huo, ili kusajihisha biashara na muingiliano wa watu katika shughuli za kiuchumi.

Mingine ni ujenzi wa daraja kubwa la Kigongo Busisi katika Ziwa Victoria lenye urefu wa kilomita 2.3 kwa gharama yah bilioni 699.2. Daraja hilo ni aina yake Afrika Mashariki na la sita Afrika kwa urefu.

Mbali ya kunufaisha Watanzania, daraja hilo pia litanufaisha nchi jirani za Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Uganda na Burundi.

Mingine ni ujenzi wa barabara za lami kutoka Tanzania na kuunganisha baadhi ya nchi katika eneo hilo na kuweka taratibu nzuri za ufanyaji biashara.

Akizungumza mwishoni mwa wiki alipokutana kwa nyakati tofauti na kufanya mazungumzo na Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, mkoani Kigoma na mkoani Geita alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni hivi karibuni, Rais Magufuli alisema ili kuimarisha biashara na mataifa mengine katika Kanda ya Maziwa Makuu na Afrika Mashariki kwa ujumla, Tanzania itanunua meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 4,000 itakayofanya shughuli zake ndani ya Ziwa Tanganyika.

Alisema meli hiyo itasafirisha na kuchukua mizigo kutoka mataifa yote yanayotumia Ziwa Tanganyika ambayo ni Tanzania, Burundi, DRC na Rwanda ambayo itaunganishwa na ziwa hilo kwa usafiri wa reli.

Mbali na meli ya mizigo, Rais Magufuli alisema Tanzania imepanga kununua meli mpya ya abiria, itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na mizigo ambayo itafanya shughuli zake katika ziwa hilo na mataifa yanayotumia ziwa hilo.

Mipango na shauku ya kuimarisha biashara katika kanda hiyo, inashajihishwa na ukuaji mkubwa wa biashara kati ya Tanzania na Burundi. Kwa mujibu wa Rais Magufuli, biashara kati ya nchi hizo mwaka 2016 ilikuwa na thamani yah bilioni 115.15.

Alisema kutokana na mahusiano mazuri kati ya Tanzania na majirani zake, mfano Burundi, hadi kufikia mwaka 2020, biashara ilikuwa hadi kufikia thamani ya zaidi yah bilioni 201.

“Mbali na hayo kituo chetu cha uwekezaji kimesajili miradi 16 ya uwekezaji kutoka Burundi, ambayo ina thamani ya dola za Marekani milioni 29.42 na imetoa ajira kwa watu zaidi ya 544,” alisema.

Rais Magufuli alisema kuna kampuni zaidi ya 10 za Tanzania, ambazo zimewekeza Burundi ambazo alizitaja kuwa ni Azam Limited, Maxcom Africa Limited, Interpetrol, Benki ya CRDB na nyinginezo.

Rais Magufuli alisema uchumi wa Burundi unaitegemea Tanzania kwa asilimia kubwa kwa sababu asilimia 95 ya mizigo yake na bidhaa zake zinasafirishwa kupitia Bandari ya Dar esalaam.

"Bidhaa za Burundi zinazopitia katika Bandari ya Dar esalaam zimekuwa zikiongezeka, miaka ya nyuma bidhaa hizo zilikuwa tani 379,704, lakini hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana Burundi ilisafirisha tani 481,081,” alisema Rais Magufuli.

Aidha, Tanzania imeiruhusu Burundi kuuza baadhi ya madini yake katika Kituo cha Biashara ya Madini mkoani Kigoma na kufungua milango kwa mataifa mengine ya Kanda ya Maziwa Makuu na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuuza madini kama dhahabu na mengine nchini Tanzania.

Hivi karibuni wakati Rais Magufuli alipokutana na Rais Museveni huko Chato mkoani Geita, alisema serikali ya Tanzania itanunua meli mpya itakayokuwa ikifanya safari zake kati ya Tanzania na Uganda kupitia Bandari ya Jinja na kupitia Bandari ya Kisumu nchini Kenya.

Chanzo: habarileo.co.tz