Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania  kuuza nafaka  Sudan Kusini

C961a4770aa9dcbf30e7791fd6aec211.jpeg Tanzania  kuuza nafaka  Sudan Kusini

Tue, 18 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TANZANIA itaanza kuuza bidhaa za nafaka ikiwamo mahindi, unga wa sembe na dona, mchele, maharagen nchini Sudani Kusini.

Hatua hiyo imekuja baada ya Bodi ya Mazao Mchanganyiko Tanzania (CPB) kwenda nchini humo kutafuta fursa za kuuza mazao hayo.

Bodi hiyo imesema imejipanga na ipo tayari kuuza mazao ya nafaka nchi humo wakati wowote kuanzia sasa kulingana na mahitaji ya nchi hiyo yenye uhitaji mkubwa wa mazao hayo.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya ujumbe wa bodi hiyo kuwasili katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, Naibu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Sudan Kusini, Salwa Monytuil alisema milango ipo wazi kwaTanzania kuuza bidhaa mbalimbali ikiwamo za nafaka nchini humo.

“Hii ni fursa kwa sisi na Tanzania kufungua milango kwa kila mmoja na kwa ulimwengu ili tuweze kusonga mbele. Ikiwa tutakubali kufanya kazi pamoja na kubadilishana maoni, basi tutasonga mbele,” alisema Monytuil .

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Biashara katika Bodi ya Mazao Mchanganyiko Tanzania, Valerian Mablangeti alisema serikali za nchi hizo mbili zimekuwa zikijadiliana kwa muda mrefu kuhusu masuala ya biashara na kwamba kama wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja.

"Ni fahari yetu kufanyika kwa mkutano huu na ni fahari kwetu kuhakikisha suala hili linakamilika. Tanzania ikiwa ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tuna mambo mengi ya kufanya ya biashara kati yetu.”

“Hakuna haja ya kwenda kufanya biashara na nchi za mbali, hakika kutakuwa na njia ya kuhakikisha wafanyabiashara kati ya Sudan Kusini na Tanzania wanafanya biashara kubwa bila ya vikwazo,” alisema Mablangeti.

Chanzo: www.habarileo.co.tz