Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kuisaidia Burundi kuingia SADC

Da62f4960649813c848e5a080a63965a Tanzania kuisaidia Burundi kuingia SADC

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi ameiahidi nchi ya Burundi kuwa Tanzania itashirikiana nayo katika harakati zake za kuomba kujiunga na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Prof Kabudi ametoa ahadi hiyo leo mkoani Kigoma kwenye mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Burundi.

Amesema Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wa kindugu baina ya nchi hizo mbili kama njia mojawapo ya kuwaenzi waasisi wake.

“Njia pekee ya kuwaenzi waasisi wa mataifa haya mawili ni kuimarisha uhusiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, kijamii na masuala ya usalama” amesema Prof Kabudi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz