Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Rwanda na Afrika Kusini zaungana na Kenya na Nigeria dawa ya kikohozi

Tanzania, Rwanda Na Afrika Kusini Zaungana Na Kenya Na Nigeria Dawa Ya Kikohozi Tanzania, Rwanda na Afrika Kusini zaungana na Kenya na Nigeria dawa ya kikohozi

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Mataifa ya Tanzania, Rwanda na Afrika Kusini yamejiunga pamoja na Kenya na Nigeria kusitisha matumizi ya dawa ya kikohozi kwa watoto kwa jina Benylin.

Hii ni kutokana na wasiwasi kuhusu usalama wake baada ya vipimo vya maabara nchini Nigeria kubaini kuwa dawa hizo za kikohozi za kampuni ya Johnson & Johnson zilikuwa na sumu.

Dawa hiyo ina kiungo ambacho uchunguzi umebaini kwamba kilisababisha vifo vya watoto nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu mwaka 2022.

Kemikali ya Diethylene glycol ni sumu kwa binadamu inapotumiwa na inaweza kusababisha figo kushindwa kufanya kazi.

Dawa ambazo zimepigwa marufuku zilitengenezwa nchini Afrika Kusini mwaka 2021 na zinatarajia kupitisha muda wake wa matumizi mwezi huu wa Aprili mwaka 2024.

Bodi ya madawa nchini Kenya imesema ya kwamba imeanzisha uchunguzi huku ikiwataka wananchi walionunua dawa hizo kuziregesha mara moja.

Chanzo: Bbc