Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Kenya Wajadili Vikwazo Visivyo vya Kiforodha

KENYA TZ?fit=660%2C330&ssl=1 Tanzania, Kenya Wajadili Vikwazo Visivyo vya Kiforodha

Thu, 27 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Tanzania, Kenya Wajadili Vikwazo Visivyo vya Kiforodha May 27, 2021 by Global Publishers



Mwenyekiti wa timu ya majadiliano ambae ni Mkurugenzi wa Mtangamano wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara – Tanzania, Ally Gugu akiongea na washiriki (hawapo pichani) wakati wataalamu hao walipokutana leo Jijini Arusha kujadili njia za kuondoa vikwazo visivyo vya kibiasha baina ya Tanzania na Kenya. Kulia ni mwenyekiti mwenza kutoka Kenya ambae ni Mkuu Kitengo cha Biashara baina ya Nchi na Nchi, Idara ya Biashara na Maendeleo ya Ujasiriamali Michael Mandu.

TIMU ya wataalamu kutoka Tanzania imekutana na timu ya wataalamu kutoka Kenya Jijini Arusha kujadili njia za kuondoa vikwazo visivyo vya kibiasha baina ya Nchi hizo kwani vimekuwa vikiathiri biashara.

Mkutano wa jana Mei 26, 2021 ni maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wa Biashara wa pande zote mbili utakaofanyika tarehe 29 Mei 2021.

Mkutano wa leo utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 28 Mei 2021 na baadaye mkutano wa Mawaziri tarehe 29 Mei 2021. Mkutano huo utahitimishwa kwa mawaziri wa Kenya na Tanzania kufanya ziara katika mpaka wa Namanga tarehe 30 Mei, 2021 kujionea shughuli za biashara zinavyofanyika katika mpaka huo.

Ujumbe wa Tanzania katika timu wataalam umeongozwa na Mkurugenzi wa Mtangamano wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Ally Gugu wakati ujumbe wa Kenya umeongozwa na Michael Mandu, Mkuu wa Biashara baina ya Nchi na Nchi, Idara ya Maendeleo ya Biashara na Ujasiriamali.

Mkutano wa wataalamu umetoa fursa ya kujadili masuala yote yanayokwamisha biashara baina ya pande zote mbili ambapo masuala yaliyowasilishwa na Kenya kujadiliwa ni pamoja na kutotoa upendeleo kwa sigara, maziwa, bidhaa za nyama, kutoka Kenya, tozo ya kuingia kwa wafanyabiashara (business pass) kufanya kazi za muda mfupi za kitaalamu.

kwa upande wa Kenya, baadhi ya masuala ambayo Tanzania imewasilisha kujadiliwa ni kuongezwa bei ya vinywaji baridi (uplifting) kutoka Tanzania, kutoza ushuru wa forodha bidhaa za glass, kuzuia mahindi kutoka Tanzania, bei kubwa ya ushuru wa stempu katika bia, kubadili mfumo wa uingizaji mizigo mikubwa ambapo gharama za uingizaji mizigo Kenya zimeongezeka na kuathiri biashara.

Katika kutekeleza maagizo ya Wakuu wa nchi (Tanzania na Kenya) mawaziri wa seka husika kutoka watakutana na kujadili juu ya vikwazo hivyo katika mkutano wao utakaofanyika tarehe 29 Mei, 2021 jijini Arusha.

Tarehe 4 – 5 Mei, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alifanya ziara rasmi nchini Kenya ambapo katika ziara hiyo Samia Hassan Suluhu na Mwenyeji wake Uhuru Kenyatta pamoja na mambo mengine, walielekeza Mawaziri wa Biashara wa pande zote wakutane na kujadili vikwazo vya kibiashara ambavyo vinaathiri biashara kwa lengo la kuviondoa.

Chanzo: globalpublishers.co.tz