Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 2 za Uranium asili zapotea

Uranium Sd Tani 2 za Uranium asili zapotea

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juhudi zinaendelea kutafuta zaidi ya tani 2 za madini ya uranium asilia yaliyoripotiwa kupotea kwenye hazina ya madini hayo huko nchini Libya, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limesema.

Msemaji wa shirika hilo aliiambia CNN kwa barua pepe kuwa: "Takriban tani 2.5 za madini ya uranium asilia, hayakupatikana wakati wa ukaguzi uliofanyika Machi 14.

"Wakaguzi wa shirika la IAEA waligundua kuwa magunia 10 yaliyokuwa na takriban tani 2.5 za madini ya uranium asilia katika mfumo wa mkusanyiko wa madini ya uranium hayakuwepo kwenye eneo lililotangazwa awali katika Jimbo la Libya.

“Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Mariano Grossi amewaalika wajumbe wa shirika hilo na maofisa wanaofanya kazi ili kubaini kilichotokea kwa uranium hiyo na ilipo sasa,” iliongeza taarifa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live