Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanasaha Donna asema huku Diamond akionekana na Zari

De3c001c9cccb39c Tanasaha Donna asema huku Diamond akionekana na Zari

Mon, 26 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Diamond Platnumz yupo Afrika Kusini kwa ajili ya kurekodi albamu mpya na alipata fursa ya kuwaona watoto wake na mzazi mwenzake Zari Hassan

- Baada ya mwanamuziki huyo kuonekana na Zari, Tanasha Donna ambaye pia amezaa na Diamond aliandika ujumbe mtandaoni na kusema wakati wake utafika

- Ujumbe wake uliwadia wakati Diamond Platnumz akisema albamu inayotarajiwa itakuwa nzito zaidi ya mwongo huu

- Ziara ya Diamond nchini Afrika Kusini inajiri wiki kadhaa baada ya yeye pia kuonekana na mtoto wa Tanasha Donna, Naseeb Junior nchini Tanzania

Tanasha Donna amejitokeza na kutoa sauti yake siku chache baada ya Diamond Platnumz kuonekana na mzazi mwenzake Zari Hassan kule Afrika Kusini.

Kupitia ujumbe aliouandika mtandaoni, mwanamziki huyo raia wa Kenya alisema anajua siku yake itafika atakapokutana na Mungu wake.

Kulingana na Tanasha, muda ukifika wa kukutana na muumba wake, hamna mtu atakayekuwa naye.

"Najua wakati wangu utakuja, mimi tu na Muumba wangu. ," Tanasha aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.



Ujumbe wake uliwadia wakati baba ya mtoto wake Diamond Platnumz alipokuwa yupo Afrika Kusini kwa ajili ya kurekodi albamu ya muziki wake.

Akiwa nchini humo, Diamond amekuwa akipata muda wa kutosha kuwa na watoto wake, ambao wanaishi na Zari Hassan ambaye ni mfanyabiashara na sosholaiti.

Ijumaa usiku, Diamond alitumia muda wake mwingi kuwa na binti yake na akamuonyesha ala za muziki na hata kuimba naye wimbo.

Kupitia video, mwanamuziki huyo aliposti video za Latifah akicheza chombo cha MIDI huku akiguna maneno ya muziki.



Diamond alielezea wakati ambapo binti yake alikuwa akicheza na chombo hicho kuwa "wakati bora zaidi".

Akichukua video ya bintiye akiwa studio ya nyumbani, Diamond ambaye yupo Afrika Kusini kwa ajili ya kurekodi albamu mpya alisema, kwa wanawe kushiriki, albamu hiyo itakuwa bora zaidi karne hii.

"Wakati mzuri kabisa ... sasa unajua itakuwa albamu babu kubwa!!," Diamond aliandika chuini ya video aliyoinasa wakati Latifah akicheza chombo cha MIDI.

Ziara ya Diamond nchini Afrika Kusini inajiri wiki kadhaa baada ya yeye pia kuonekana na mtoto wa Tanasha Donna, Naseeb Junior nchini Tanzania.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke