Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takribani watu milioni 8 wameambukizwa Corona Afrika

Image (2).png Maambukizi ya Corona Afrika

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu takribani Milioni 8 wameambukizwa Corona Afrika Bara la Afrika linakabiliwa na maambukizi ya haraka ya ugonjwa wa Corona unaosababishwa na virusi vya COVID-19 ambapo mpaka kufikia leo September 9, 2021 imeripotiwa kuwa kuna maambukizi Milioni 7,972,013.

Kwa mujibu wa taarifa za Chuo Kikuu cha John Hopkins cha nchi Marekani, Bara la Afrika limeendelea kuandamwa na visa vya aina tofauti za kirusi cha COVID-19. Mpaka sasa Virusi aina 4 vimeripotiwa katika mataifa mbalimbali barani hapa ambapo tayari kirusi cha Delta kimesambaa kwenye nchi 25 za Afrika.

Taarifa ya CNN pia iliyotoka mwezi August 25, 2021 imesema kuwa karibia asilimia 80% ya vifo vyote vya Corona vinavyotokea barani Afrika vimetokana na kirusi cha Delta.

Kumekuwa na lawama za moja kwa moja kwa serikali za Afrika kutokana na kushindwa kutoa huduma ya chanjo kwa haraka pamoja na namna ya kupambana na janga hili. Baadhi ya nchi zimelegeza masharti ya kujikinga na Corona huku nchi nyingine zikitoa lawama kwa mataifa makubwa kwa kushindwa kutoa misaada ya chanjo kwenye nchi masikini.

Afrika imeripoti vifo zaidi ya 200,000 mpaka sasa huku idadi ya waliochanjwa mpaka sasa ikiwa ni ndogo kwa chini ya Asilimia 8 ya idadi ya watu bilioni 1.3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live