Takribani tani moja za kokeini zimepotea mikononi mwa polisi
Mkuu wa polisi nchini Guinea-Bissau alisema siku ya Alhamisi kwamba karibu tani moja ya kokeini iliyokamatwa na mamlaka mwishoni mwa mwaka jana "imetoweka hewani".
Domingos Monteiro, mkurugenzi wa polisi wa mahakama katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, alisema kuwa maafisa walikamata kilo 980 za cocaine mnamo Novemba 2021, katika operesheni ya magendo ambayo maelezo yake bado hayajafahamika.
"Lakini kilo 975 zilitoweka hewani," mkuu wa polisi aliiambia AFP, akiongeza kuwa polisi na maafisa wa vikosi vya usalama wanashukiwa kumiliki kokeini.
Afisa mmoja wa polisi amekamatwa, Monteio alisema.
Siku ya Alhamisi, kesi inayohusu usafirishaji haramu wa tani moja ya kokeini ilianza katika mji mkuu Bissau, mwandishi wa habari wa AFP aliyekuwepo alisema, ambapo washukiwa saba kati ya tisa walifikishwa mahakamani.
Bado haijafahamika iwapo wanachama wa vikosi vya usalama ni miongoni mwa washukiwa.