Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takriban watu 6 wameuawa kwa kupigwa risasi katika basi nchini Ghana

Ghanaaaa Risasiiii Takriban watu 6 wameuawa kwa kupigwa risasi katika basi nchini Ghana

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu sita wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine saba wamejeruhiwa wakati kundi moja la watu wenye silaha wasiojulikana kuwashambulia watu hao kwenye basi katika mkoa wa mmoja wa kaskazini mashariki mwa Ghana.

Hamza Amadu, afisa mtendaji mkuu wa manispaa ya Bawku amethibirisha habari hiyo na kusema kuwa, tukio hilo limetokewa wakati basi hilo lilipokuwa linasafiri kutoka Bawku katika mkoa wa Upper East, wa kaskazini mashariki mwa Ghana.

Amesema, waliofariki ni pamoja na wanaume wawili na wanawake wanne, na waliojeruhiwa wanapokea matibabu katika hospitali mbili za karibu na eneo hilo.

Ameongeza kuwa" "Usalama umeimarishwa kwa doria za wanajeshi na askari polisi, huku amri ya kutotoka nje ikiwa nayo imewekwa ili kudhibiti mienendo ya watu nyakati za usiku."

Vilevile amesema kuwa, operesheni ya pamoja ya polisi na jeshi inaendelea kuwasaka na kuwakamata wahusika wa uhalifu huo wa kutisha.

Eneo hilo liko umbali wa kilomita chache kutoka mpaka na Burkina Faso, na hivi karibuni limekumbwa na machafuko ya kutumia silaha kutokana na mzozo wa muda mrefu baina ya machifu na vitendo vingine vya uhalifu.

Shambulio hilo limetokea wiki moja baada ya lile la Jumatano iliyopita wakati watu wenye silaha wasiojulikana walipowashambulia na kuwaua watu wawili katika kitongoji hicho.

Amadu pia amesema kuwa, hivi sasa kuna hofu ya kuongezeka mivutano hasa kutokana na kuwa, wiki iliyopita wanajeshi wa serikali waliwaua watu watatu na kutangaza kuwa walilazimika kuwafyatulia risasi watu hao ili kujilinda. Tukio hilo lilitokea Januari 19, 2024.

Hivi karibuni pia, maafisa wa Tume ya Uchaguzi ya Ghana (EC) walilazimika kusimamisha zoezi la uandikishaji wapiga kura ya uchaguzi mdogo katika eneo hilo la Bawku, ili kulinda wafanyikazi wake na vifaa kutokana na mvutano mkubwa uliopo kwenye eneo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live