Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takriban watu 40 wameuawa shambulio la kambi ya DR Congo

Takriban Watu 40 Wameuawa Shambulio La Kambi Ya DR Congo Takriban watu 40 wameuawa shambulio la kambi ya DR Congo

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Maafisa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanasema kuwa takriban watu 40 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na kundi lenye silaha kwenye kambi ya waliokimbia makazi yao.

Kiongozi wa kikabila katika mkoa wa Ituri mashariki alisema idadi ya waliopoteza maisha inaweza kuongezeka kwani vibanda vingi katika kambi hiyo vimeteketezwa na miili zaidi inaweza kuwa kwenye mabaki .

Mashambulizi ya Jumatatu yamelaumiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Codeco kutoka kabila la Lendu, ambalo lina uhasama wa muda mrefu na wafugaji wa Hema.

Pia imelaumiwa kwa shambulio la Jumamosi ambapo watu saba walifariki.

Chanzo: Bbc