Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takriban watu 20 wameuawa katika shambulizi Cameroon

Wanaoshukiwa Majambazi Wawateka Karibu Raia 40 Nchini Chad Na Cameroon Takriban watu 20 wameuawa katika shambulizi Cameroon

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu karibu 20 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na kundi la watu wanaotaka kujitenga nchini Cameroon. Habari zinasema kuwa shambulio hilo lilitekelezwa usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Egbekaw, magharibi mwa Cameroon; eneo yanapojiri mapigano makali kati ya waasi na vikosi vya jeshi la serikali kwa miaka saba sasa.

Watu wasiopungua 20 ambao ni wanaume, wanawake na watoto, wameuawa katika shambulio hilo linalodaiwa kufanywa na kundi la watu wanaotaka kujitenga wanaozungumza lugha ya Kiingereza huko Cameroon. Watu wengine 10 wamejeruhiwa vibaya na sasa wamelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Maeneo ya Cameroon yanayozungumza Kiingereza hasa Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi, yamekumbwa na migogoro tangu watu wanaotaka kujitenga nchini humo walipotangaza uhuru wao mwaka wa 2017. Kundi la wanaopigania kujitenga nchini Cameroon

Inaelezwa kuwa, watu hawa walichukua hatua hiyo kufuatia kile walichokitaja kuwa miongo kadhaa ya kubaguliwa na jamii ya raia walio wengi wa Cameroon wanaozungumza lugha ya Kifaransa.

Rais Paul Biya wa Cameroon mwenye umri wa miaka 90 ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa miaka 41, ametupilia mbali miito inayomtaka kuruhusu kujitawala jamii hiyo ya waliowachache.

Hali hii ya mgogoro imesababisha watu zaidi ya 6,000 kupoteza maisha na wengine zaidi ya milioni moja kuhama makazi yao.

Kundi hilo la vijana waliokuwa na silaha linalopigania kujitenga huko Cameroon, liliwashambula raia usiku wa kuamkia jana huko Egbekewe ambapo habari nyingine zinasema kuwa watu 23 wameuawa na nyumba karibu 15 zimechomwa moto. Hii ni katika hali ambayo, tangu mwishoni mwa 2016, mzozo mbaya unahusisha makundi ya watu wanaopigania kujitenga huko Cameroon na vikosi vya usalama, huku kila upande ukituhumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kuwa yametenda uhalifu dhidi ya raia, katika mikoa ya Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi, inayokaliwa zaidi na watu wachache wanaozungumza Kiingereza kwenye nchi hiyo ya Afrika ya Kati yenye watu wengi wanaozungumza Kifaransa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live