Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takriban robo ya wanachi DRC wakabiliwa na njaa

Wakimbizi Congo Drc.png Takriban robo ya wanachi DRC wakabiliwa na njaa

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limetangaza kuwa takriban watu milioni 23.4 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yaani karibu robo ya wakazi wa nchi hiyo wanakabiliwa na kiwango fulani cha janga la njaa.

WFP imesema katika ripoti yake kwamba, tatizo la njaa linalosababishwa na migogoro huko DRC linazidi kuwa kubwa huku ghasia na mapigano katika majimbo ya mashariki mwa nchi hiyo yakiongezeka na kulazimisha watu kukimbia tena makazi yao.

Taarifa hiyo ya WFP imeongeza kuwa, raia wengi wanaendelea kutafuta hifadhi katika mji wa Goma ambao ni makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini na kupelekea kuongezeka migogoro kutokana na uhaba wa chakula na hivyo kusababisha mfumuko usio wa kawaida wa bei za bidhaa muhimu hasa chakula katika masoko ya Goma. Mji wa Goma

Katika ziara yake ya hivi karibuni ya kuutembelea mji wa Goma, Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, Cindy McCain, aliona kwa karibu hali mbaya inavyoendelea kuwatesa mamilioni ya watu walioathiriwa na migogoro hiyo.

Baada ya ziara hiyo McCain alisema: "Mji wa Goma umezungukwa na makumi ya maelfu ya makazi ya muda, na idadi inaongezeka kila siku. Watu waliokimbia makazi yao wamejazana karibu na Goma na wanahitaji chakula, maji safi na usafi wa mazingira. WFP inahitaji msaada wa wafadhili ili kuongeza kasi ya huduma zake kwa watu wanaoishi katika kambi za wakimbizi kabla ya kuchelewa."

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, WFP inahitaji dola milioni 548.5 za Kimarekani ili kuweza kuendelea kutoa huduma kwa wakimibzi huko DRC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live