Takriban watu milioni 282 barani Afrika - karibu 20% ya wakazi wa bara hilo - hawana lishe bora, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Afrika na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa.
Ripoti hiyo ya pamoja pia ilifichua kuwa idadi ya Waafrika wenye lishe duni imeongezeka kwa watu milioni 57 tangu kuanza kwa janga la Covid-19, kuashiria kuongezeka kwa chakula barani Afrika.
"Watu wengi wa Afrika - karibu 78%, au zaidi ya watu bilioni moja - bado hawawezi kumudu chakula chenye afya, ikilinganishwa na asilimia 42 katika ngazi ya kimataifa, na idadi inaongezeka," mashirika yaliongeza.
Ripoti hiyo imehusisha kuenea kwa kutoweza kumudu chakula chenye afya na kuongezeka kwa gharama za chakula katika miaka ya hivi karibuni.
Mashirika hayo pia yalisema takribani asilimia 30 ya watoto chini ya miaka mitano barani humo wamedumaa kutokana na utapiamlo.