Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tajiri wa Algeria ahukumiwa kifungo alichomalizia mahabusu

Tajiri wa Algeria ahukumiwa kifungo alichomalizia mahabusu

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Algiers. Tajiri namba moja nchini Algeria, Issad Rebrab (74) ameachiwa huru baada ya mahakama kumhukumu kwenda miezi sita, muda ambao tayari alikuwa ameshautumikia akiwa rumande.

Tajiri huyo alihukumiwa Jumatano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kodi, benki na forodha.

Waendesha mashtaka waliomba mfanyabiashara huyo aliyekamatwa Aprili pamoja na matajiri kadhaa kwa tuhuma za ufisadi, afungwe jela mwaka mmoja.

Lakini hakimu alimhukumu Rebrab kifungo hicho, ambacho kimeisha na kuachiwa kwa kuwa alikuwa ameshatumikia miezi minane akiwa rumande.

Mbali ma kifungi hicho, Rebrab alitakiwa kulipa faini dinars 1.383 bilioni (Sh26.7 bilioni).

Kamopuni yake ya Cevital ilipigwa faini 2.766 dinars(Sh53.6 bilioni)

Alishtakiwa kwa kukiuka sheria za ubadilishaji wa fedha za kigeni, uhamishaji fedha, kughushi na kutoa taarifa za uongo za forodha.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes, Rebrab anatajwa kama ndiye tajiri namba moja nchini Algeria na wa sita Afrika akiwa na utajiri wa dola za Marekani 3.9 bilioni kwa mwaka jana.

Kampuni yake ya Cevital inayoajiri watu 18,000  inazalisha vifaa vya elektroniki, chuma na vyakula. Hivi karibuni alifungua biashara nchini Ufaransa.

Wakati biashara zake zilishamiri katika kipindi cha Rais Abdelaziz Bouteflika, Rebrab aliunga mkono maandamano yaliyoung’oa utawala wake mwezi Aprili.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz