Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taharuki! Afukua kaburi la mkewe ili auze shamba

Kaburi M Afukua kaburi la mkewe ili auze shamba

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamume mwenye umri wa miaka 76, amewashangaza wanakijiji wa Mumero, eneo la Timau katika kaunti ya Meru baada ya kufukua mwili wa mke wake ili kuuza shamba lake.

Mwanamume huyo aliyetambulika kwa jina Robert Marangu anasemekana kuomba usaidizi wa wakazi wa kijiji hicho kufukua mwili wa marehemu mke wake Joyce Kanyua aliyefariki 2021.

Hii ni baada ya mtu aliyetaka kununu kipande hicho cha ardhi kusema hangeweza kununua ikiwa na kaburi.

Akithibitisha kisa hicho, chifu wa kata ya Kithithina, Lucy Mutwiri alisema kuwa alitembelea eneo hilo na kupata tayari kaburi limehamishwa kutoka mahali lilipokuwa.

"Ni jambo la kushangaza ambalo limefanyika katika eneo langu na ndipo wakazi waliniambia kuhusu yaliyofanyika. Nilizuru eneo hilo na kubaini kwamba kaburi lilikuwa lishabadilishwa kutoka mahali lilipokuwa." alinukuliwa chifu huyo na gazeti la Taifa Leo.

Chifu huyo aliongeza akisema kuwa mzee huyo alisaidiwa kuufukua mwili huo na mjukuu wake na majirani wake wawili.

"Aliamua kuuza ardhi yake alikokuwa amemzika mkewe na kuona kuwa uamuzi wa busara aliokuwa nao ni kuondoa mahali mwili huo ulipokuwa," aliongeza Mutwiri.

Mkuu wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI), katika eneo hilo Joseph Wambua alibainishwa kwamba waliohusika kwenye ufukuzi huo wamekamatwa na wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Timau wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Kwingineko polisi katika kijiji cha Ebwambwa kaunti ya Kakamega wamemuokoa mwanamke mwenye umri wa miaka 58, ambaye alikuwa amevamiwa na umati wenye hasira kuhusiana na kifo tatanishi cha mwanawe.

Katika tukio hilo la Jumanne, Januari 24, mwili wa mwanawe Eunice Andanje, Ezekiel Munanga, 32, ulipatikana ukioza nyumbani kwake.

Akithibitisha kisa hicho, chifu wa eneo hilo Fanuel Lumumba alisema Andanje alitofautiana na Munanga kuhusu pakiti ya kilo 2 ya unga wa mahindi kabla ya kifo chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live