Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tahadhari yatolewa kuhusu ugonjwa wa kipindupindu Afrika Kusini

Tahadhari Yatolewa Kuhusu Ugonjwa Wa Kipindupindu Afrika Kusini Tahadhari yatolewa kuhusu ugonjwa wa kipindupindu Afrika Kusini

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: Voa

Mamlaka ya afya nchini Afrika Kusini inawataka wakazi wa jimbo la Gauteng kuwa waangalifu kuhusu vinywaji wanavyotumia huku idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa kipindupindu ikiongezeka hadi karibu watu 50.

Vyama vya wafanyakazi na vikundi vya kijamii vimeitaka serikali kuingilia kati zaidi ili kuboresha ubora wa maji.

Katika muda wa wiki sita zilizopita vifo vingi vimetokea katika eneo la Hammanskraal, ambapo wakaazi wanasema wamehangaika kwa wiki kadhaa kupata maji safi, lakini kumekuwa na visa vya ugonjwa huo kote nchini.

Katika maeneo mengi, maji ya bomba si salama na watu wanalazimika kutegemea matanki ya serikali.

Kipindupindu, ambacho huenezwa zaidi na chakula na maji yaliyochafuliwa, husababisha kuhara na kutapika sana na kinaweza kuua ndani ya saa chache kisipotibiwa.

Chanzo: Voa