Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taarifa ya mashambulizi ya anga Tigray yapingwa vikali na Serikali

Soldiers Ef Taarifa ya mashambulizi ya anga Tigray yapingwa vikali na Serikali

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Ethiopia imetupilia mbali malalamiko ya mashambulizi ya kianga katika mkoa wa Tigray yaliyotolewa katika ripoti ya chama kikuu cha upinzani cha mkoani hapo cha TLPF, wanadiplomasia pamoja na watetezi wa haki za bianadamu Oktoba 18,2021.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya Ethiopia inaeleza kuwa hakukuwa na mashambulizi yoyote kwa wakazi wa eneo la Makele lilipo mkoani hapo.

"Hakukuwa na mashambulizi kwa wananchi wa Makele, mnajua kuwa Makele ni sehemu ya nchi, ni sehemu ya makazi ya wanachi wetu, ripoti hii ni ya uongo hakuna ukweli hapa" Amesema Legesse Tulu Msemaji Mkuu wa Serikali.

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Tigray amesema kuwa hospitali hiyo imepokea miili ya watu watatu waliofariki kwenye shambulio la anga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live