Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taarifa ya Benki ya Dunia inaonesha watu milioni 86 watakimbia makazi

Niger Change Watu milioni 86 kuyakimbia makazi yao Nigeria

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Dunia imetoa tahdhari ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea dunia huku ikiimulika nchi ya Nigeria ambayo imetajwa kuwa kwenye hatari zaidi huku watu milioni 86 wakikadiriwa kuyakimbia makazi yao nchini humo kufika mwaka 2050.

Ripoti hiyo imeongeza kusema kuwa watu milioni 216 wanatarajiwa kuyakimbia makazi yao ulimwenguni kufuatia mabadiliko hayo ya hali ya hewa.

Aidha ripoti hiyo ambayo imeandikwa kwa kichwa cha habari cha 'Mabadiliko ya hali ya hewa yatakayo waladhimu watu milioni 216 kuyakimbia makazi yao mwaka 2050' imetolewa na kuchapishwa na Benki hiyo ya dunia.

"Ripoti ya Benki ya Dunia inabainisha mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yataongeza wimbi la watu kuyahama makazi yao na inakadiriwa watu milioni 216 duniani kote watalazimika kuyakimbia makazi yao kwa mwaka 2050" imesema ripoti hiyo.

Hata hivyo imeongeza kusema kuwa madhara ya mabadiliko haya yanatarajiwa kuanza mapema kwaka 2030 na kuendelea hadi 2050.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live