Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taa za kuongoza ndege zaibiwa Nigeria

Airport Runway Lights Taa za kuongoza ndege zaibiwa Nigeria

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wezi wameiba mfumo wa taa kwenye barabara za kuruka na kutua ndege katika moja ya viwanja vya ndege nchini Nigeria, ikiwa ni miezi michache baada ya taa hizo kuwekwa.

Mamlaka ya viwanja wa ndege nchini humo imesema kuwa uchunguzi umeanza ili kuwakamata wahusika pamoja na kurejesha vilivyoibwa kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Mohammed jijini Lagos.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vimedai kuwa watumishi wa uwanja wa ndege walihusika katika wizi huo.

Taa hizo zilifungwa Novemba 2022 ili kuwezesha ndege kuruka na kutua wakati wote, tofauti na awali ambapo safari za ndege kwenye uwanja huo zilikoma pindi giza linapoingia.

Kutokana na wizi huo, ndege zinazofanya safari za ndani ya nchi zililazimika kutua eneo la ndege za kimataifa, na abiria walichukua usafiri wa gari kurudi takribani kilomita nne kwenye jengo linalohudumia abiria wa ndani.

Imeelezwa kuwa wezi hao walitumia mwanya wa barabara hiyo kuwa imefungwa kwa muda kwa ajili ya marekebisho, wakaiba taa hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live