Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TP Mazembe yasubiri wabaya wake Ligi ya Mabingwa

94579 Pic+mazembe TP Mazembe yasubiri wabaya wake Ligi ya Mabingwa

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Droo ya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, itafanyika leo huko Cairo, Misri kuanzia saa 2.00 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki ikihusisha jumla ya timu nane.

Hafla ya uchezeshaji wa dro hiyo ambayo itasimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), itafanyika katika hoteli ya Hilton Pyramids Golf iliyopo jijini Cairo.

Taratibu za uchezeshaji wa droo hiyo ni kwamba timu nne zilizoongoza makundi manne ya mashindano hayo ambazo ni TP Mazembe (DR Congo), Etoile Du Sahel (Tunisia), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) na Esperance (Tunisia) zitawekwa katika chungu cha kwanza wakati chungu cha pili kitakuwa na timu za Zamalek na Al Ahly (Misri) pamoja na Wydad Casablanca (Morocco) ambapo zile zilizoongoza kila moja itapangwa kukutana na zile zilizoshika nafasi ya pili.

Pia kwa mujibu wa muongozo wa uchezeshaji droo hiyo, katika hatua ya robo fainali, timu ambazo zinatoka katika nchi moja zinaweza kupangwa kukutana zenyewe kwa zenyewe ikiwa hilo litatokea.

TP Mazembe imetinga hatua hiyo baada kuongoza kundi A huku mshindi wake wa pili akiwa ni Zamalek wakati kinara wa kundi B ni Etoile Du Sahel na aliyeshika nafasi ya pili ni Al Ahly ya Misri.

Mamelodi Sundowns imeongoza kundi C mbele ya walioshika nafasi ya pili, Wydad Casablanca na kundi D limeongozwa na Esperance na waliofuata wakiwa ni Raja Casablanca.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz