Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TP Mazembe kuhusu kumsajili nyota wa Aston Villa

TP MZEA TP Mazembe kuhusu kumsajili nyota wa Aston Villa

Wed, 13 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya soka ya TP Mazembe ya nchini DR Congo, imekanusha tetesi za kumsajili kiungo wa zamani wa klabu za Lyon na Aston Villa Jean Makoun raia wa Cameroon.

Kupitia taarifa yake TP Mazembe wamesema hakuna ukweli kuhusu tetesi hizo ambazo zimekuwa zikielezwa kupitia mitandao mbalimbali ya Cameroon na DRC.

''Hatujamsajili na wala hatuna mpango na Jean Makoun, ni mchezaji mzuri lakini kikosi chetu hakina uhitaji wa huduma yake kwasasa'', imeeleza sehemu ya taarifa ya klabu hiyo.

Jean Makoun alifanya vizuri kwenye soka la Ulaya akiwa na klabu ya Lyon kati ya mwaka 2008 hadi 2011 kisha Aston Villa mwaka 2011 hadi 2013. Lakini pia amechezea vilabu tofauti tofauti vya Ulaya ikiwemo Lille ya Ufaransa na Olympiacos ya Ugiriki.

Kwasasa Jean Makoun akiwa na umri wa miaka 36 hana klabu hivyo akisajiliwa atakuwa ni mchezaji huru na huenda timu isipate gharama kubwa kupata sahihi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live