Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TCAA yatoa sababu Ndege za Kenya kuzuiwa

IMG 4791?fit=1080%2C720 TCAA yatoa sababu Ndege za Kenya kuzuiwa

Thu, 27 Aug 2020 Chanzo: dar24.com

Mamlaka ya Usimamizi wa Anga nchini (TCAA), imesema kuwa sababu iliyopelekea kuzifungia Ndege 3 za Kenya kuja nchini ni kutokana na Kenya kuendelea kuiwekea vikwazo vizito Tanzania na raia wake kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 27, 2020, na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio

“Tumezifungia Ndege za Kenya kwa sababu Tanzania bado inawekewa vikwazo vizito kule kwahiyo na sisi tumerithishwa guilty bila sababu”, amesema Hamza

Ili kumaliza hili suala ni mazungumzo tu na wao watakapokuwa tayari sisi tutakuwa tayari kwa mazungumzo maana sisi hatuna tatizo la kuzungumza na kuweka mambo sawa lakini lazima wao wawe na utashi wa kufanya hivyo“, ameongeza.

Wabunge washtukia pesa za Covid-19 kupigwa, watoa siku 60Ndege zilizowekewa zuio ni Air Kenya Express, Fly 540 na Safarilink Aviation ikiwa ni siku chache tu tangu Kenya ilipotoa orodha ya nchi 130 ambazo raia wake wataruhusiwa kuingia nchini humo na hawatokaa karantini huku Tanzania ikiwekwa kando.

Rwanda yamsaka ‘mpelelezi wake’ kwa tuhuma za mauaji ya kimbariMoto wateketeza mabweni shule ya African Muslim

Chanzo: dar24.com