Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TB Joshua azikwa Lagos

F4a35ae0b9cf5d374007707c670ef1f9.jpeg TB Joshua azikwa Lagos

Fri, 9 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWINJILISTI Maarufu nchini Nigeria TB Joshua amezikwa huko Lagos baada ya wiki moja ya ibada za mazishi.

Maelfu ya waombolezaji walihudhuria ibada ya mazishi katika Sinagogi lake, Kanisa la Mataifa Yote (SCOAN) katika eneo la Ikotun huko Lagos.

Temitope Balogun Joshua, alifariki akiwa na umri wa miaka 57. Alifariki mnamo Juni 5 baada ya kuugua kwa muda mfupi, kanisa lilisema.

TB Joshua aliheshimiwa na watu kutoka ulimwenguni kote na makumi ya maelfu ya watu walihudhuria huduma zake za kila wiki.

Kuinuka kwa mhubiri huyo mwenye haiba mwishoni mwa miaka ya 1990 sanjari na mlipuko wa vipindi vya "miujiza" vilivyofanywa kwenye Runinga ya Nigeria na wachungaji anuwai.

Kanisa lake lilidai kuponya kila aina ya magonjwa, pamoja na VVU / Ukimwi na kuvutia watu kutoka kote ulimwenguni.

Chanzo: www.habarileo.co.tz