Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Suti za Kaunda, zinazopendwa na Rais Ruto, zapigwa marufuku bungeni Kenya

Suti Za Kaunda, Zinazopendwa Na Rais Ruto, Zapigwa Marufuku Bungeni Kenya Suti za Kaunda, zinazopendwa na Rais Ruto, zapigwa marufuku bungeni Kenya

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Bunge la Kenya limepiga marufuku uvaaji wa kaunda suti, vazi lililopewa jina la aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Kenneth Kaunda, ndani ya jengo hilo.

Spika wa Bunge, Moses Wetangula alisema suti za Kaunda, pamoja na nguo za asili za Kiafrika, hazikubaliki.

Rais wa Kenya William Ruto mara nyingi huvaa kwenye hafla rasmi. Hii imefanya suti ya Kaunda, koti la safari na suruali inayofanana na koti kupendwa na wanasiasa.

Suti hiyo imepewa jina la marehemu rais wa Zambia ambaye alipenda kuvaa nguo hizo na kuzifanya kuwa maarufu miongoni mwa viongozi wa kisiasa kote Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Suti hiyo, ambayo pia inajulikana kama suti ya Mao Zedong, haina ukosi na mara nyingi ya mikono mifupi.

Siku Jumanne, Bw Wetangula alisema uamuzi wake wa kupiga marufuku suti hiyo ulitokana na mitindo iliyoibuka ambayo ilikiuka kanuni za mavazi ya bunge.

Alibainisha kuwa kanuni sahihi ya mavazi kwa wanaume "inamaanisha kanzu, ukosi, tai, shati ya mikono mirefu, suruali ndefu, soksi, viatu, au sare ya huduma". "Kwa wanawake mavazi rasmi, au nadhifu ya kawaida hutumika.

Sketi na nguo zinapaswa kuwa chini ya urefu wa goti na zenye heshima. Blauzi zisizo na mikono haziruhusiwi," alisema.

Suti ya Kaunda ilishawahi kuruhusiwa bungeni na baadhi ya wabunge wamekuwa wakijulikana kwa kuvaa mara nyingi.

Bw Wetangula alikiri kwamba suti hizi "zilivumiliwa kwa namna fulani" hapo awali lakini sasa ni wakati wa kukomesha hilo huku kukiwa na tishio kwa kanuni za mavazi ya bunge.

Suti hiyo ya Kaunda imevuma kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya hivi karibuni, baada ya Bw Ruto kuanza kuvalia katika hafla rasmi.

Kupigwa marufuku kwa suti hiyo kumezua hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakishangaa ni kwa nini "vazi la Kiafrika" litapigwa marufuku na bunge la Afrika, huku wengine wakiunga mkono.

Baadhi pia wamekejeli marufuku hiyo, wakisema suti ya Kaunda sasa itakuwa ya rais pekee. "Wakati tu unapofikiri umeyaona yote... nadhani suti za Kaunda sasa zimetengwa kwa ajili ya [rais]," alisema mtumiaji wa mtandao wa kijamii kwenye X (zamani Twitter).

Chanzo: Bbc