Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sunak: Mpango wa wahamiaji Rwanda upo pale pale

Kagame Amshutumu Tshisekedi Kutafuta Sababu Ya Rwanda Kuahirisha Uchaguzi Congo Sunak: Mpango wa wahamiaji Rwanda upo pale pale

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameahidi kuwa awamu ya kwanza ya mpango wa kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda utaanza katika muda wa wiki 10 hadi 12 zijazo.

Sunak aidha ameahidi kutatua mvutano uliopo kwenye bunge kuhusu mpango kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwishoni mwa mwaka huu.

Kauli ya Sunak imekuja baada ya wiki iliopita kuapa kuwa bunge litaendelea na vikao vyake hadi sheria hiyo ipitishwe.

Sunak amelitaka bunge la House of Lords liache kuzuia sheria inayoruhusu mamlaka kuwatuma baadhi ya waomba hifadhi nchini Rwanda, huku akijaribu kufanikisha ahadi yake ya kuzuia kuwasili wa wahamiaji haramu nchini Uingereza.

Kiongozi huyo licha ya kutoa ahadi hiyo, amekosa kueleza ni wahamiaji wangapi wanaotarajiwa kutumwa nchini Rwanda katika kipindi cha miezi ijayo.

Muswada huo ulikuwa umekwama kwa muda wa miezi miwili wakati wabunge wakijaribu kuujadili.

Baada ya kutia saini makubaliano mapya na Rwanda kuimarisha usalama wa waomba hifadhi, serikali ya Uingereza ilipendekeza sheria mpya ya kuitangaza Rwanda kama nchi salama kwa waomba hifadhi.

Mpango huo umekuwa ukikabiliwa na changamoto si haba, baadhi ya mashirika ya kutetea haki za binadamu yakisema ni kinyume na sheria.

Mamlaka nchini Rwanda kwa upande wake imekuwa imeendelea kushikilia msimamo kuwa nchi yake ni salama kwa watafuta hifadhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live