Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Suluhu Kenya: Serikali, upinzani waunda kamati watu 10

Kenyatta Erss Suluhu Kenya: Serikali, upinzani waunda kamati watu 10

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muungano wa upinzani wa Azimio la Umoja nchini Kenya, umesema umekubaliana na Serikali, kuunda kamati ya watu 10, ili kujadili na kutatua changamoto zinazoikabili nchi hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kiongozi wa Muungano wa upinzani Bungeni, Opiyo Wandayi, ambaye amefafanua kuwa maafikiano hayo yamekuja baada ya kushauriana na wenzao wa Muungano wa Kenya Kwanza.

Amesema , mazungumzo hayo yataongozwa na kusimamiwa na Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo na yanalenga kutatua changamoto kati ya Serikali na upinzani kwa manufaa ya wananchi wa Kenya.

Katika mazungumzo hayo, kila upande utatoa watu watano, kuunda kamati hiyo na tayari taarifa hiyo pia imethibitishwa na upande wa Serikali, kupitia kiongozi wake bungeni, Kimani Ichung’wah ingawa haijafahamiki ni lini mazungumzo hayo yataanza rasmi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live