Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudani Kusini yatokomeza polio

A0fb2119f5b69b3007258f36bebc8ec0 Sudani Kusini yatokomeza polio

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SUDAN Kusini imetangazwa kutokuwa na maambukizi ya virusi vya polio, ikiungana na nchi nyingine za Afrika zilizotokomeza ugonjwa huo na kufanya bara hilo kutokuwa na ugonjwa huo.

Kutokomezwa kwa ugonjwa huo nchini humo kumethibitishwa na Tume ya Uthibitishaji ya Kanda ya Afrika katika kutokomeza ugonjwa wa polio (ARCC) baada ya kutangazwa rasmi na Shirika la Afya Duniani (WHO).

ARCC ni chombo huru ambacho kiliteuliwa mwaka 1998 na Mkurugenzi wa WHO Afrika kusimamia mchakato wa uthibitishaji maeneo yasiyo na ugonjwa huo.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) Sudan Kusini, Shirika la Afya Duniani (WHO) Sudan Kusini na Wizara ya Afya, imeeleza kuwa, uamuzi wa ARCC ulifanywa kwa kuzingatia mapitio ya kina ya takwimu mbalimbali, ikijumuisha uchunguzi, chanjo ya kawaida na takwimu za kampeni ya polio na baada ya ziara ya ukaguzi uliofanywa Januari mwaka huu na ujumbe wa ARCC.

Taarifa hiyo ilisema wajumbe wa ARCC walisafiri kwenda Warrap, Jonglei na Ikweta Magharibi ili kuangalia jinsi mpango wa polio unavyofanya kazi nchini humo.

"Kukubalika kwa nchi hii kutokuwa na virusi vya polio ni hatua muhimu katika historia ya nchi hii katika kuboresha afya ya umma," alisema Mwenyekiti wa Tume ya Udhibitisho Sudan Kusini, Dk Rose Mapour.

Chanzo: habarileo.co.tz