Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan yawafukuza wanadiplomasia 15 wa UAE

Sasa Si Wakati Wa Mazungumzo   Mkuu Wa Jeshi La Sudan Sudan yawafukuza wanadiplomasia 15 wa UAE

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sudan imewaamuru wanadiplomasia 15 wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) kuondoka nchini humo huku baadhi ya maafisa wa Sudan wakidai kwamba nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi inaunga mkono wapiganaji waasi wa Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF)

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Jumapili ilimwita Balozi Mdogo wa UAE Badria Alshihi na kumfahamisha kuhusu uamuzi wa kuwafukuza wanadiplomasia hao 15.

Hakuna sababu rasmi iliyotolewa ya kufukuzwa, lakini hatua hiyo imekuja huku kukiongezeka mvutano kati ya Sudan na Muungano wa Falme za Kiarabu kuhusu tetesi kuwa UAE inawaunga mkono wapiganaji hao wa RSF.

Wiki iliyopita, Yassir Alatta, mjumbe wa Baraza tawala la Sudan, aliishutumu UAE kwa kulipatia kundi hilo la kijeshi silaha na vifaa kupitia nchi jirani, zikiwemo Uganda, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad.

Hivi karibuni Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilitangaza kuwa zaidi ya watu 12,000 wameuawa nchini Sudan katika vita vya wenywe kwa wenyewe vilivyoanza Aprili 15 mwaka huu huku hali ikiendelea kuwa mbaya.

Sudan imekumbwa na vita kati ya Jeshi la Kitaifa likiongozwa Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa Baraza la Utawala la nchi hiyo, na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) vikiongozwa na jenerali muasi Mohammad Hamdan Dagalo (Hemedti).

Hitilafu kati ya al-Burhan na Dagalo zilijitokeza baada ya kusainiwa mkataba wa kuunda uongozi wa kipindi cha mpito ili kukabidhiwa madaraka kwa raia. Dagalo anataka wapiganaji wa RSF waingizwe jeshini lakini al Burhan anapinga pendekezo hilo. Mikataba kadhaa ya kusitisha mapigano iliyosimamiwa na Saudia imeshindwa kukomesha ghasia hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live