Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan yavifunga kwa muda vituo vya televisheni

Sudan Yavifunga Kwa Muda Vituo Vya Televisheni Sudan yavifunga kwa muda vituo vya televisheni

Wed, 3 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Sudan imevifungia vituo vitatu vya Televisheni vya Pan-Arab, ikivishutumu kwa "ripoti zisizo za kitaalamu na uchapishaji unaodhuru".

Sky News Arabia inayomilikiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Al Arabiya na Al Hadath inayomilikiwa na Saudi Arabia, ambazo zimeathiriwa na agizo hilo, zimeripoti kwa mapana kuhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe na machafuko ya kisiasa nchini Sudan.

Kusimamishwa huko kulichochewa na watangazaji hao "kutojitolea kwa taaluma na uwazi unaohitajika" na kushindwa kwao kuhuisha leseni zao, Waziri wa Habari Graham Abdel Gader alinukuliwa akisema.

Kusimamishwa kwa Sky News Arabia inayofadhiliwa na UAE pia kulitokana na "uchapishaji mbaya", kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Al Hadath na Al Arabiya walisema hawakufahamishwa rasmi kuhusu kusimamishwa kazi na mara nyingi wamehuisha leseni zao.

Kusimamishwa huko kumekuja siku chache baada ya wizara ya mambo ya nje ya Sudan kuishutumu Sky News Arabia kwa kupeperusha bandia za wanamgambo.

Kituo hicho kilitumia video ya shambulio la kundi la wanamgambo wa al-Shabab nchini Somalia mwaka 2016 kuhusu makundi ya wanamgambo wanaodaiwa kupigana pamoja na Wanajeshi wa Sudan.

Uhusiano kati ya Sudan na UAE umedorora baada ya jeshi la Sudan na vyombo vya habari vya Magharibi kushutumu UAE kwa kusambaza silaha kwa Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF) katika mzozo wa karibu mwaka mzima.

Muungano wa Wanahabari wa Sudan (SJS) ulitaja uamuzi huo "ukiukaji wa wazi wa uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari".

Chanzo: Bbc