Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan yatiwa hofu na kutumwa kwa wanajeshi 'hatari'

Sudan Yatiwa Hofu Na Kutumwa Kwa Wanajeshi 'hatari' Sudan yatiwa hofu na kutumwa kwa wanajeshi 'hatari'

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Hali ya wasiwasi imetanda nchini Sudan baada ya jeshi kushutumu kikosi chenye nguvu cha kijeshi kwa kukusanya wanajeshi katika mji mkuu, Khartoum na miji mingine, na kupeleka wanajeshi bila idhini ya uongozi wa vikosi vya jeshi.

Mzozo kuhusu kuunganishwa kwa Vikosi vya (RSF) katika jeshi umezidisha mzozo wa kisiasa nchini Sudan, miaka minne baada ya jeshi kumpindua rais wa muda mrefu Omar al-Bashir.

Katika taarifa iliyotolewa mapema leo kwenye Shirika la Habari la Sudan (Suna), Jeshi la Sudan (SAF) lilionya kwamba kutumwa kwa kikosi cha RSF "ni ukiukaji wa wazi wa sheria" na "bila shaka kutasababisha migawanyiko na mivutano zaidi ambayo inaweza kusababisha kuharibika kwa usalama wa nchi”.

Jeshi liliongeza kuwa uwepo mkubwa wa kikosi cha RSF "ulizua hofu na wasiwasi miongoni mwa raia, kuzidisha hatari za usalama, na kuongeza mvutano kati ya vikosi vya kawaida".

Maendeleo hayo yanazua hofu ya makabiliano ya kijeshi kati ya jeshi na RSF yakichochewa na mzozo wa madaraka kati ya kiongozi wa jeshi la wanamgambo Jenerali Mohamed Hadan Dagalo na kiongozi wa mapinduzi ya Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Jana, jeshi la SAF liliripotiwa kuizuia kikosi cha RSF kusimama katika eneo karibu na Uwanja wa Ndege wa Merowe kaskazini mwa Sudan, ambao ni mwenyeji wa Jeshi la Anga la Sudan.

Chanzo: Bbc