Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan yataka ujumbe wa UN uondoke nchini humo mara moja

Sudan Kusini Inaweza Ikaathirika Ikiwa Vita Vya Sudan Sudan yataka ujumbe wa UN uondoke nchini humo mara moja

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sudan imeutaka Umoja wa Mataifa jana, kuuondoa haraka ujumbe wake wa UNITAMS nchini humo.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Ali Sadeq ameliandikia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuutaka ujumbe huo wa UNITAMS kuondoka nchini humo mara moja.

Katika barua hiyo iliyotumwa kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na kusambazwa kwa baraza hilo, Sadeq ameuhakikishia Umoja huo kwamba serikali ya Sudan imejitolea kushirikiana kikamilifu na baraza hilo pamoja na makao makuu ya Umoja huo wa Mataifa.

Sadeq amesema kuwa madhumuni ya kuanzisha misheni hiyo ilikuwa kusaidia serikali ya mpito ya Sudan baada ya mapinduzi ya Desemba 2018 na kuongeza kuwa utendakazi wa ujumbe huo katika kutekeleza malengo yake ni wa kukatisha tamaa.

Alipoulizwa kuhusu uamuzi huo wa Sudan, msemaji wa Guterres Stephane Dujarric, amesema barua hiyo imepokelewa na kuwasilishwa kwa baraza hilo la usalama.

Uhusiano kati ya serikali ya Sudan na Umoja wa Mataifa umekuwa mbovu tangu vita vilipozuka nchini humo Aprili 15.

Volker Perthes, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan alijiuzulu mwezi Septemba, zaidi ya miezi mitatu baada ya serikali ya Sudan kutangaza kuwa hatakiwa nchini humo. Rais wa Sudan, Abdel Fattah al-Burhan alimshutumu kwa kuchochea mzozo nchini Sudan.

Sudan imekuwa katika hali ya mzozo wa silaha ambao uliibuka Aprili 15 kati ya Jeshi la Kitaifa a Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Sudan (RSF). Maelefu ya watu wameuawa katika vita hivyo na malaki ya wengine kuwa wakimbizi nje na ndani ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live