Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan yataka kurejeshewa uanachama kabla ya kukubali upatanishi wa AU

Sudan Yataka Kurejeshewa Uanachama Kabla Ya Kukubali Upatanishi Wa AU Sudan yataka kurejeshewa uanachama kabla ya kukubali upatanishi wa AU

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan anasema Sudan itazingatia pendekezo la Umoja wa Afrika la kumaliza mzozo huo ikiwa muungano huo utarejesha uanachama wake kamili.

AU ilisimamisha Sudan kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 25 Oktoba 2021.

Jenerali Burhan alikutana na wajumbe wa Jopo la Ngazi ya Juu la AU lililoundwa hivi karibuni kuhusu Utatuzi wa Mzozo nchini Sudan, likiongozwa na Mohamed Ibn Chambas, Jumapili.

Jopo hilo la watu watatu lilianzishwa na Tume ya AU mwezi Januari ili kuwezesha mazungumzo, kurejesha utulivu wa kikatiba na kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wa Sudan na jumuiya ya kimataifa kuelekea amani ya kudumu.

Taarifa kwenye ukurasa wa Facebook wa Baraza Kuu la Sudan ilisema Jenerali Burhan alionyesha "imani ya Sudan kwa AU na uwezekano wa kupatikana kwa suluhu ambayo inaweza kumaliza vita, lakini ikiwa tu serikali itarejeshewa uanachama wake kamili".

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Ibn Chambas alisisitiza dhamira ya AU ya kusaidia kumaliza mzozo na kurejesha utulivu nchini Sudan.

Chanzo: Bbc