Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan yakataa wito wa Umoja wa Mataifa wa kuleta kikosi cha amani kuwalinda raia

Sudan Yakataa Wito Wa Umoja Wa Mataifa Wa Kuleta Kikosi Cha Amani Kuwalinda Raia.png Sudan yakataa wito wa Umoja wa Mataifa wa kuleta kikosi cha amani kuwalinda raia

Mon, 9 Sep 2024 Chanzo: Bbc

Serikali inayoongozwa na jeshi la Sudan imekataa wito ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kutathmini uwezekano wa kutumwa kwa kikosi cha kimataifa ili kuwalinda raia dhidi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo.

Pande zinazopigana nchini Sudan zimefanya ukiukaji "wa kutisha" wa haki za binadamu dhidi ya raia, ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliripoti.

Maelfu ya watu wameuawa na karibu milioni nane wamekimbia makazi yao tangu mzozo ulipozuka Aprili 2023 kati ya jeshi na Kikosi cha (RSF).

Pande hizo mbili zilikuwa zimefanya mapinduzi, lakini baadaye zikatofautiana, na kuitumbukiza Sudan katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

"Kutokana na kushindwa kwa pande zinazopigana kuwaacha raia, ni muhimu kwamba kikosi huru na kisichopendelea upande wowote chenye mamlaka ya kulinda raia kipelekwe bila kuchelewa," kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa, Chande Othman, alisema.

Ujumbe huo wa kutafuta ukweli pia ulitoa wito wa kuwekewa vikwazo vya silaha kwa pande zote zinazohusika katika mzozo huo.

Iliripoti matokeo yake baada ya kupata ushuhuda wa moja kwa moja kutoka kwa manusura 182, wanafamilia na mashahidi waliojionea ukatili nchini Sudan.

Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unashutumiwa kwa kuunga mkono RSF kwa fedha na silaha - jambo ambalo inakanusha - huku Saudi Arabia ikisemekana kuwa na uhusiano wa karibu na serikali ya Sudan.

Wizara ya mambo ya nje ya Sudan ilisema serikali ilikataa mapendekezo ya ujumbe wa kutafuta ukweli kwa "jumla".

Chanzo: Bbc