Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan yakabiliwa na kukatika kwa huduma za intaneti

Sudan Yakabiliwa Na Kukatika Kwa Huduma Za Intaneti Sudan yakabiliwa na kukatika kwa huduma za intaneti

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Sudan imekubwa na kukatika kwa mtandao huku wengi wakilaumu kundi la wanamgambo wanaopambana na jeshi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi 10 nchini humo.

Kikosicha (RSF) kimekana kuhusika.

NetBlocks, shirika linalofuatilia uhuru wa mtandao, lilisema kwenye X, kumekuwa na "kuporomoka kwa muunganisho wa intaneti" nchini Sudan.

Inakuja wakati kundi la wadukuzi ambao ni wanaharakati wa Sudan kuilenga Uganda kwa kumkaribisha kiongozi wa RSF, Mohamed Hamdan Dagalo.

NetBlocks ilisema imepata usumbufu kwa huduma za watoa huduma za intaneti Uganda Telecom na MTN, ingawa ripota wa BBC katika mji mkuu Kampala alisema hakuona matatizo yoyote.

Nchini Sudan, baadhi ya watu wameripoti kutoweza kupata mtandao tangu Ijumaa lakini hali imekuwa mbaya zaidi tangu wakati huo.

Vyombo vya habari vinayoungwa mkono na serikali vimeilaumu RSF.

Hata hivyo, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Sudan Tribune, afisa wa RSF alishutumu jeshi kwa kutoa maagizo ya moja kwa moja ya kukata mawasiliano katika sehemu za majimbo ya Darfur, Kordofan, Khartoum na Al-Jazirah, ambayo kwa kiasi kikubwa yako chini ya udhibiti wa kundi la wanamgambo.

NetBlocks ilisema Jumatano kwamba mojawapo ya waendeshaji wakubwa wa simu nchini Sudan, Zain, "kwa kiasi kikubwa haikuwa na mtandao"

Chanzo: Bbc