Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan yakabiliwa na hali mbaya ya njaa na utapiamlo

Watoto Sudan Sudan Sudan yakabiliwa na hali mbaya ya njaa na utapiamlo

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Njaa na utapiamlo vinaenea kote nchini Sudan, mwaka moja tangu kuzuka kwa vita kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Usaiidizi wa Haraka (RSF) huku ikiwa hakuna dalili ya vita kusitishwa hivi karibuni.

Katika baadhi ya kambi za watu waliokoseshwa makaazi huko Darfur Kaskazini, wakaazi, madaktari na wafanyakazi wa misaada wanasema kuwa, watu wamelazimika kula udongo na majani.

Kwa mujibu wa shirika linaloangazia usalama wa chakula, IPC, takriban watu milioni 18 nchini Sudan, ikiwa ni zaidi ya theluthi moja ya watu, wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Wakati huo huo zaidi ya watu nusu milioni wanalazimika kuvuka mpaka karibu kila siku na kuingia Sudan Kusini kwa kutumia vivuko mbalimbali vya mpaka.

Idadi ya wanaokimbia inazidi kuongezeka huku mzozo ukiendelea, watu wengi wanafika wakiwa wamedhoofika, wakiw na njaa na waliokata tamaa.

Wafanyakazi wa misaada walioko kwenye eneo hilo wanasema idadi kubwa ya watu wanaowasili kutoka Sudan huingia katika kijiji cha Renk nchini Sudan Kusini kila siku na hii inasababisha changamoto kubwa kwa juhudi za kibinadamu katika kusimamia na kutoa msaada.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kwamba janga la njaa nchini Sudan litazidi kuwa mbaya kama watu wake hawataendelea kupatiwa misaada ya mara kwa mara ya kibinadamu kadiri inavyowezekana.

Wakati huo huo Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umeeleza kuwa kuna majanga yanayoingiliana ya hali mbaya ya hewa mashariki na kusini mwa Afrika, ambapo mwaka jana maeneo hayo mawili yaliathiriwa na dhoruba, mafuriko, joto na ukame.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live