Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan yaitaka UN kusitisha shughuli za tume yake ya siasa nchini humo

Sudan Siasa Jeshi Sudan yaitaka UN kusitisha shughuli za tume yake ya siasa nchini humo

Sat, 18 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka za Sudan zimeutaka umoja wa Mataifa, kusitisha mara moja shughuli za tume yake ya kisiasa nchini humo, hii ni kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na kaimu waziri wa mambo ya nje wa taifa hilo, Ali Sadeq.

Uhusiano wa Khartoum na Umoja wa Mataifa unaendelea kuwa mbaya zaidi, hatua hii ikidhiirisha mvutano uliopo.

Kwa mujibu wa barua iliyovuja ambayo Khartoum imeliandikia baraza la usalama, inasema Sudan imeamua kumaliza majukumu ya walinda amani wa umoja huo (Unitams) mara moja.

Kwa sasa baraza hilo linajukumu la kuamua hatma ya kikosi cha UN ambacho kilitumwa nchini Sudan mwaka wa 2020 kwa lengo la kulisaidia taifa hilo kurejea kwenye utawala wa kiraia, mpango ambao umeonekana kukwama tangu mwezi oktoba mwaka wa 2021.

Sudan imekuwa ikikabiliwa na mapigano tangu tarehe 15 ya mwezi Aprili kati ya wapiganaji wa RSF na jeshi la taifa hilo. Tangu wakati huo, karibia watu elfu tisa wameuawa, zaidi ya wengine milioni tano wakitoroka makazi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live